Log in
updated 5:40 PM UTC, Apr 16, 2017

TAIFA LAMUAGA CAPTAIN JOHN DAMIANO MTOKAMBALI KOMBA

Hivi ndivyo gwiji la nyimbo za hamasa, umoja na mshikamano wa kitaifa hayati Captain John Damiano Mtokambali Komba alivyohitimisha miaka yake 61 hapa duniani alipolazwa kwenye nyumba yake ya milele pale kijijini Lithuli, wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma siku ya tarehe 3 Machi 2015. Captain Komba, Mbunge na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM atakumbukwa daima na ataishi daima kupitia tenzi zake. Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Ruvuma Mhashamu John Ndimbo akiongoza usharika wa waumini wa imani mbalimbali kumsindikiza kwa sala marehemu Captain John Komba.