Log in
updated 5:40 PM UTC, Apr 16, 2017

ESCROW: MHIMILI WA BUNGE WAPEWA JUKUMU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ameielekeza mihimili mikuu ya dola kuwachukulia hatua stahiki wale wote waliohusishwa na kashfa ya Escrow. Akiwahutubia watanzania kupia wazee wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Dimond Jubilee jana,  Rais ameuelekeza mhimili wa Mahakama kupitia kwa Jaji Mkuu kujadili na kuona ni hatua zipi zichukuliwe dhidi ya viongozi wa mahakama waliohusishwa.

Aidha, Rais ameutaka mhimili wa Bunge kupitia kwa Spika uone ni hatua zipi za kinidhamu zinazofaa dhidi ya viongozi wa Kamati za Kudumu za Bunge waliohusishwa na sakata hili. Kwa upande wa mhimili wa serikali Rais amesema tayari Mwanasheria Mkuu, jaji Fredrick Werema, ameshajiuzulu mwenyewe. Aidha, amechukua hatua ya kumwajibisha waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka. Ameongeza kuwa uchunguzi unafanyika na hivi karibuni atachukua hatua dhidi ya waliosalia akiwemo waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bwana Eliakimu Maswi.

  • Published in ikulu

KB AELEKEZA TARATIBU ZA KUWASILISHA TAARIFA BUNGENI

Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah (kushoto) akitoa ushauri  kwenye Kamati ya Uongozi jinsi ya kuwasilishwa Bungeni taarifa mbalimbali leo kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb).

AWEPA KUWAJENGEA UWEZO WABUNGE WA TANZANIA

Ujumbe wa AWEPA ukiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Titus Kamani (Mb) katika Ofisi za Bunge Dar es Salaam hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengini wamekubaliana kuwajengea uwezo wabunge wa Tanzania katika maeneo ya Mifugo na Uvuvi.

  • Published in ikulu

JK AMWAPISHA MASAJU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemwapisha Jaji George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye shughuli iliyofanyika Ikulu leo.

Jaji Masaju anachukua nafasi ya Jaji Fredrick Werema aliyejiuzulu wadhifa huo mapema mwezi uliopita kufuatia maazimio ya Bunge yaliyohitimisha mgogoro wa fedha za IPTL na Tanesco kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

  • Published in ikulu

Spika akutana na mabalozi ujumbe wa awepa

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda (Mb) akimkabidhi Balozi wa Urusi hapa nchini, Bwana Alexander Ranniekh, zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro hivi karibuni mara baada ya Balozi huyo kufika Ofisini kwa Spika kumuaga baada ya kumaliza utumishi wake wa uwakilishi hapa nchini.

Balozi Ranniekh amesema daima atawakumbuka watanzania kwa ukarimu wao kwa wageni.

Kamati ya Uongozi ya Bunge yakutana

Mweneykiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (kulia) akiendesha kikao cha Kamati ya Uongozi mara baada kuahirisha kikao cha Bunge. Hapa anatoa ufafanuzi kwa baadhi mambo yalijitokeza ambapo pamoja na mambo mengine amesema taarifa ya CAG kuhusu IPTL itakabidhiwa kwa Waziri Mkuu naye ataikabidhi kwa Spika wa Bunge.

MASAJU AAPISHWA KUWA MWANASHERIA MKUU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemwapisha Jaji George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye shughuli iliyofanyika Ikulu leo.

Jaji Masaju anachukua nafasi ya Jaji Fredrick Werema aliyejiuzulu wadhifa huo mapema mwezi uliopita kufuatia maazimio ya Bunge yaliyohitimisha mgogoro wa fedha za IPTL na Tanesco kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

  • Published in ikulu

Taarifa maalum ya CAG kuhusu IPTL mikononi mwa PAC

Naibu Spika Mhe. Job Ndugai akiwakabidhi Mwenyekiti Mhe. Zitto Zuberi Kabwe na Makamu Mwenyekiti Mhe. Deo Filikunjombe wote wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma taarifa ya CAG kuhusu ukaguzi maalum kufuatia taarifa za gazeti la Citizen la mwezi Machi 2014.

  • Published in ikulu
Subscribe to this RSS feed